3.2 KISWAHILI (102) 3.2.1 Kiswahili Paper 1 (102/1) 1 Lazima: Wewe ni meneja katika kampuni ya Jitihada ambapo pamekuwa na visa vya ukiukaji wa maadili ya kikazi. Waandikie wafanyakazi memo kuwaonya dhidi ya jambo hili. 2 “Rununu (simutamba) imeleta athari mbaya katika jamii.” Jadili. 3 Andika kisa kitakachodhihirisha maana ya methali: Usitukane wakunga na uzazi ungalipo. 4 Tunga kisa kinachoanza kwa maneno yafuatayo: Moyo wangu ulidunda kwa matarajio makuu … 11 3.2.2 Kiswahili Paper 2 (102/2) 1 UFAHAMU: (Alama 15) Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Gari lake kuukuu lilikuwa linapambana na barabara yenye mashimo yaliyoshiba na kutapika maji ya mvua ambayo sasa ilikuwa inaanza kupusa. Japo daima alipambana na usukani kunako mashimo haya yaliyotosha kuitwa magenge, alishukuru kwa hali hii. Vipi angeweza kulidhibiti gari lake hili kwenye barabara iliyosakafiwa nayo ikahitimu? Magurudumu haya yaliyong’ara kama upara wa shaibu aliyekula chumvi hadi ikamwogopa yangetii uelekezi wake? Mara ngapi gari hili limetaka kumwasi barabarani? Haya yalikuwa baadhi ya maswali yaliyompitikia akilini. Hakujitakilifu kutaka kuyapa mji maana mara ile mawazo yake yalitekwa na kubwagwa katika nchi ya mbali – nchi ambayo sasa aliiona kama sinema akilini mwake. Alipofika nyumbani aliliegesha gari lake na kufululiza ndani. Siku mbili zilikuwa zimepita akiwa pale kazini. Madaktari kama yeye hawakuwa wengi. Alikuwa miongoni mwa madaktari wenye ujuzi katika hospitali hii ya kitaifa. Wenzake wengi walikuwa wamehamia ughaibuni walikokwenda kutafuta maisha. Mshahara wao wa mkia wa mbuzi uliwasukuma na kuwatema nje ya nchi yao. Wengi wa waliohamia ng’ambo waliona vigumu kubaki katika ajira ambayo kivuno chake kilishindwa kumvusha mtu hata nusu ya kwanza ya mwezi. Malalamishi ya kulilia ujira wa heshima yaligonga kwenye masikio yaliyotiwa zege. Na kweli wanavyosema, mwenye macho haambiwi tazama. Basi walitazama hapa na pale wakaona penye mianya ya matumaini, nao wakaiandama. Hadi leo hii hamna la mno lililofanyika. Ndiyo maana Daktari Tabibu anarudi nyumbani tangu kuingia kazini hiyo juzi alfajiri. Hafanyi kwa kuwa katosheka, maana pia yeye ana dukuduku. Ana shaka ya mustakabali wake ikiwa mazingira ni haya ya kumsoza, maana umri nao unazidi kumla. Japo anatia na kutoa, mizani ya hesabu yake imeasi ulinganifu. Daktari Tabibu waama ni mfungwa. Ametekwa na kuzuiwa katika kupenda na kuchukia mambo. Ni kama mti uliodumaa. Anatamani barabara nzuri za lami. Anatamani mshahara wa kumwezesha kukidhi mahitaji yake na kutimiza majukumu yake ya kimsingi. Jana amesema na rafiki yake aliye ng’ambo kwa simu ambayo sasa imetulia mkabala naye. Ingawa mwenzake huyu alikuwa mchangamfu na kumdokolea hali ya maisha ya kuridhisha kule ugenini kama vile wanataaluma kuenziwa, yapo vilevile yaliyomtia unyonge moyoni. Upweke ndio uliomtia fukuto kuu. Licha ya hela zote hizo za kupigiwa mfano, watu hawana muda wa kutembeleana na kujuliana hali au hata kukutana tu mkahawani wakashiriki mlo. Eti ni kila mtu na hamsini zake. Halafu ipo changamoto ya hali ya hewa. Baridi ya ng’ambo haifanyi mzaha katika kumtafuna mtu. Ni hali tofauti na ile aliyoizoea. 12 Daktari Tabibu alizitia kauli za rafiki yake kwenye mizani ya moyo wake. Akawaza ikiwa kweli si bora kulemazwa na mzizimo ugenini badala ya kuishi katika kinamasi cha kuumbuliwa […]
Read More »